Back to top

Majambazi 6 wajeruhiwa kwa Risasi Temeke

22 July 2022
Share

Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Muliro Jumanne Muliro amesema Jeshi hilo limewajeruhi kwa risasi majambazi sita usiku wa kuamkia leo katika barabara ya Mbozi iliyopo Keko wilayani Temeke ambapo amebainisha kuwa majambazi hao wapatao 9 wakiwa na silaha 1 aina ya pistol, mapanga 4 na funguo nyingi za kutendea uhalifu, waliwatishia walinzi kwa silaha na kuwafunga kamba, baadaye wakaingiza gari aina ya Hiace kwenye ghala ili kuiba vipuri vya magari.
.
Hata hivyo, Kamanda Muliro amesema walipopata taarifa za tukio hilo walifika haraka na kulikuta kundi hilo, likaanza kuwatishia Askari kwa silaha, Polisi nao wakajihami.