Back to top

Majengo hatarishi ya shule ya wasichana Songea kubomolewa.

21 December 2019
Share

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bi. Christina Mndeme ameagiza majengo yaliyo hatarini kuwaangukia wanafunzi  katika shule ya wasichana ya Songea yabomolewe ili kulinda usalama wa wanafunzi.

Bi. Mndeme ametoa maagizo hayo baada ya kutembele shule ya wasichana ya Songea kukagua ukarabati unaoendelea ambapo ameunda tume kuchunguza majengo hayo  na mengine kabla ya kufikia maamuzi ya kubomoa.

Mkuu wa shule ya wasichana ya  Songea mwalimu Tupoke Ngwala  amesema alisita kuyapokea majengo hayo  ambayo hayatumiki  kwa masomo bali wanafunzi  wanayatumia kufanyia maombi.