Majeruhi wengine 7 wa ajali ya Moto Morogoro waliokuwa wakipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wamefariki.
Akizungumza na ITV Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma MNH, Aminieli Aligaesha amesema kuwa idadi ya vifo vilivyotokea kwenye hospitali hiyo ya muhimbili mpaka sasa ni watu 21, ambapo kwa siku ya jana walikuwa watu 6 na kufanya idadi kufikia watu 14 hivyo ongezeko hilo la watu 7 ambao walikuwa wanapatiwa matibabu hospitalini hapo ndilo limeongeza idadi ya watu waliofariki na kufikia hao 21.
Amesema kati ya wagonjwa 46 ambao waliwapokea katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kuwapatia matibabu wamekufa 21 hivyo wamebaki na wagonjwa 25 kati yao 16 wapo ICU huku wagonjwa 9 wakiwa katika wodi ya Sewahaji.
Aligaesha amesema bado wanaendelea na jitihada za kuwahudumia majeruhi hao, ambapo amebainisha kuwa wananchi ambao walikuwa wakichangia damu kwa ajili ya kusaidia majeruhi hao wamefanikiwa kupata lita 500.