Back to top

MAJI BWAWA LA NYUMBA YA MUNGU YAPUNGUA

02 February 2022
Share


Maji katika Bwawa la nyumba ya Mungu mkoani Kilimanjaro yamepungua kutoka mita za ujazo 689 hadi kufikia 685 kutokana na ukame ambao umesababishwa na mvua za vuli kuchelewa kunyesha na hivyo kusababisha kituo za uzalishaji umeme kuagizwa kupunguza mashine za uzalishaji umeme katika bwawa hilo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bonde la Pangani Mhandisi Segule Segule ameyasema hayo wakati wadau wa usimamizi wa raslimali za maji katika kidakio cha mto kikuletwa kutoka mikoa ya Arusha na Kilimanjaro walipokutana Moshi kwa ajili ya kuweka mikakati ya kutunza na kulinda vyanzo vya maji.

Amesema uharibifu wa mazingira kwenye vyanzo vya maji umesababishwa baadhi ya mito iliyokuwa inatiririsha maji katika bwawa hilo kukauka na kwamba wanategemea endapo mvua zitanyesha kuna uwezekano wa bwawa hilo kurejea katika hali yake ya kawaida.