Idadi ya watu wanaoingia nchini kupitia mpaka wa Namanga imeongezeka jambo linalosababisha msongamano mkubwa na pia mahitaji ya vifaa vya uchunguzi na upimaji wa virusi vya Corona.
Watendaji wa kituo hicho wamemweleza waziri wa afya Mhe.Ummy Mwalimu aliyetembelea kituo hicho kuwa kwa sasa watu kati ya 300 hadi 500 wanapita katika kituo hicho kwa siku.
Akizungumzia changamoto hiyo waziri Mhe.Ummy Mwalimu pamoja na kuahidi kufanyia kazi changamoto hiyo amewaomba wananchi kutoa ushirikiano hasa wa kutoa taarifa za watu wanaoingia kupitia njia za panya.
Tatizo la mahitaji ya vifaa vinavyolenga kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona pia imeelezwa na mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ambaye amemuomba waziri Ummy kuangalia uwezekano wa kuweka mashine ya kubaini virusi hivyo katika jiji la Arusha.
Kwa sasa watu sampuil za watu wanaohofiwa kuwa na maambukizi virusi vya Corona hulazimika kusafirishwa hadi jijini Dar es Salam ambako ndiko iliko maabara yenye uwezo wa kupima virusi hivyo.