Back to top

Maporomoko ya Sunda kivutio kikubwa cha utalii Ruvuma.

23 August 2019
Share

Maporomoko ya Sunda yaliyoko katika mto Ruvuma pembezoni mwa msitu Mwambesi wilayani Tunduru mkoani Ruvuma yamekuwa kivutio kikubwa cha utalii ambapo yameanza kutembelewa na watalii kutoka ulaya.

Afisa utalii wa kanda ya Kusini Bi. Deborah Mwakanosya amesema kuwa mto Ruvuma una vivutio vingi vya utalii ikiwemo maporomoko ya Sunda lakini pia mto huo umezungukwa na msitu  wa Mwambesi wenye wanyama mbalImbali wakiwemo tembo.

Afisa maliasili wa mkoa wa Ruvuma Bw.Africanus Challe amesema kuwa wamejipanga kuyaboresha maporomoko hayo ikiwa ni pamoja na kuboresha njia za kuingilia ili yaweze kufahamika zaidi kimataifa.

Meneja wa miradi wa shirika la PAMS Foundation shirika lililoratibu ujio wa watalii 22 kutembelea maporomoko ya Sunda  katika mto Ruvuma Bw. Max Jenes amesema kuwa wamejipanga kuutangaza zaidi mto Ruvuma huku watalii wakifurahia mwonekano mzuri wa mto Ruvuma.