Back to top

Mawakala wa pembejeo waiomba serikali kudhibiti viuatilifu feki

22 September 2019
Share

Chama cha mawakala wa pembejeo za kilimo na mifugo mkoa wa Arusha kimeiomba serikali kuweka sera na sheria inayotekelezeka katika kusimamia tatizo la  uingizwaji wa viuatilifu visivyokidhi viwango kinyemela nchini na kusababisha hasara kubwa kwa wasambazaji na wakulima.
 
 
Wakizungumza wilayani Arumeru  wakati wa mafunzo  juu ya matumizi sahihi ya pembejeo na viuatilifu mawakala hao wanasema ni vyema ukawekwa utaratibu endelevu na mazingira ya kuwafikia wakulima ili wawe makini wanapokutana na viuatilifu visivyofaa.
 
Bwana Moses Mabula ni mwakilishi  kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha ambaye anawaasa mawakala hao kuhakikisha kuwa elimu ya matumizi sahihi ya pembejeo na viuatilifu wanayoipata inawafikia wakulima.
 
Chama hicho cha mawakala kimeanzishwa mahsusi kuwaunganisha watoa huduma hao ili waweze kutoa huduma itakayoleta tija katika uzalishaji.