![](https://www.itv.co.tz/sites/default/files/styles/large/public/field/image/je_0.jpg?itok=bPE1Yuri)
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya NMuungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hafla ya Mazishi ya Kitaifa ya Rais wa Zamani wa Finland, Hayati Martti Ahtisaari iliyofanyika Helsinki tarehe 10 Novemba 2023.
Wakati wa kutoa salamu za pole, Rais Kikwete alisema kuwa Rais Samia anatoa salamu za rambirambi kwa Rais wa Findland, Mhe. Sauli Niinistö, Familia ya Marehemu na watu wote wa Finland kufuatia kifo cha kiongozi huyo mkubwa duniani.
Rais Kikwete aliungana na viongozi mbalimbali walioshiriki mazishi hayo wakimwemo Rais wa Kosovo, Mhe. Vyosa Osmani na Rais wa Namibia, Mhe. Hage Geingob na kummwagia sifa Hayati Martti Ahtisaari kwamba alikuwa kiongozi mwenye maono na mpenda amani duniani.
Hayati Martti Ahtisaari aliwahi kuwa Balozi wa Finland nchini Tanzania kuanzia mwaka 1973 hadi 1976 na alikuwa Rais wa Finland kuanzia mwaka 1994 hadi 2000.