![](https://www.itv.co.tz/sites/default/files/styles/large/public/field/image/pingu%20kgm%20viungo.jpg?itok=xQqHsBw1)
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma ACP Filemon Makungu amesema Jeshi hilo linamshikilia Taimu Kagoma mwenye umri wa miaka 39 mkazi wa Kijiji cha Gwanumpu wilayani Kakonko baada ya kukutwa na viungo vinavyodhaniwa kuwa vya binadamu ikiwemo fuvu la kichwa, mfupa wa taya na mifupa mingine ya binadamu.
.
Ambapo, Kamanda huyo amebainisha kuwa matukio hayo yamekuwa yakijirudia kutokana na imani za kishirikina.