Ukaguzi wa mbegu uliyofanywa na taasisi ya kudhibiti ubora wa mbegu nchini TOSCK katika mikoa ya lindi na mtwara umebaini uwepo wa mbegu feki za ufuta katika baadhi ya maduka yanayouza mbegu hizo, hali inayowakatisha tamaa wakulima wa zao hilo kuandaa mashamba hasa kipindi hiki cha upandaji wa zao hilo.
.
Akizungumza mara baada kufanya ukaguzi wa mbegu katika maduka yanayouza mbegu mbalimbali ikiwemo ya ufuta na mahindi mkaguzi wa mbegu kanda ya kusini Bw. Diksoni Rwabulalala amesema wapo baadhi ya wafanyabishara wamekuwa wakiuza mbegu feki hali wakijua kufanya hivyo ni kosa.
.
Amesema katika ukaguzi uliyofanyika katika mkoa wa lindi na mtwara yapo baadhi ya maduka yamebainika kuuza mbegu feki na baadhi yao kufungiwa kufanya biashara hiyo.
.
Amesema uuzaji wa mbegu feki za ufuta umechangia baadhi ya wakulima kugoma kuendelea kulima zao hilo kutokana na kupata hasara kila mwaka pia ametumia fursa hiyo kuwaonya wafanyabiashara wanaouza mbegu kununua bidhaa hiyo kwenye makampuni pasipo kupewa risiti jambo ambalo amesema ni kosa kisheria.
.
Hata hivyo amesema taasisi hiyo itaendelea kutoa elimu kwa wauza maduka ya mbegu ili wauze mbegu zenye ubora na zilizothibitishwa na taasisi hiyo.
.
Kwa upande wao wauzaji wa maduka ya mbegu wameomba elimu iendelee kutolewa kwani wakati mwingine makampuni ya mbegu yanawauzia mbegu zisizofaa na hivyo kuangukia kwenye mkono wa sheria.