Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru mwaka 2019 Bw.Mzee Mkongea Ally amemuweka mahabu meneja wa wakala wa bara bara za vijijni na mjini wa halmashauri ya wilaya ya Madaba Bw. Razaro Kitomari baada ya kudanganya kuhusu mradi barabara huku akikataa kuweka jiwe la msingi kwenye mradi huo na mradi wa jengo la ofisi ya halmashauri ya Madaba kutokana na kutokidhi vigezo.
Mradi mwingine uliokataliwa kuwekewa jiwe la msingi na Mwenge wa uhuru ni mradi wa jengo la ofisi ya halmashauri ya wilaya ya Madaba kutokana na kushindwa kukidhi vigezo ambapo vielelezo vya mradi huo amekabidhiwa afisa wa taasisi ya kupambana na rushwa TAKUKURU kwa ufuatiliaji zaidi.
Hata hivyo Mwenge wa uhuru umezindua mradi wa maji katika kijiji cha Lilondo na mradi wa darasa katika shule ya msingi Kibrang’oma.