Idara ya uhamiaji katika mkoani Kagera imemkamata mfanyabiashara raia wa Uganda, Frank Mpuuga akiwa katika harakati za kukamilisha taratibu za kuomba kitambulisho cha taifa.
Aidha idara hiyo pia inamshikilia Swalehe Athumani Mtanzania anayedaiwa kumuingiza kinyemela nchini mfanyabiashara huyo na kumpa mbinu za kuomba kitambulisho hicho.
Baada ya kupekuliwa mfanyabiashara huyo alikutwa na hati ya kusafiria ya Uganda.
Mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti ametoa onyo kwa wale wote wenye nia ya kujipatia vitambumbulisho vya taifa wakati sio watanzania na ameagiza watu wawili waliokamatwa wachukuliwe hatua kali ili liwe fundisho kwa wengine.