Back to top

Michezo ya kubahatisha kuunganishwa na TEHAMA 'kudhibiti urahibu'.

13 November 2019
Share

Naibu waziri wa fedha  na Mipango Dk.Ashatu Kijaji amesema Serikali iko mbioni kuunganisha michezo yote ya kubahatisha katika mfumo wa tehama ili kurahisisha ili kukabiliana na athari hasi zinazoambatana na michezo ya kubahatisha.

Akiongea Bungeni wakati wa  kipindi cha maswali na majibu ameema ili kukabiliana na athari hasi zinazoambatana na michezo ya kubahatisha serikali imejenga mfumo wa Tehama wa kusimamia mfumo wa mapato  na kuratibu mienendo ya wachezaji kwa nia ya kukabiliana na urahibu wa michezo hiyo kutoa elimu kwa umma kuhusu athari hasi za mchezo huo na kudhibitiuendeshaji holela wa michezo ya kubahatisha.