
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Jerry Silaa, amewataka wanafamilia wote walio na migogoro ya ardhi inayohusisha wana ndugu waimalize kifamialia kwa kufungua mirathi pindi wapendwa wao wanapofariki ili kuwa na msimamizi wa mali za marehemu aliyeaminiwa na familia.
Waziri Silaa ameyasema hayo wakati alipotembelea eneo la familia ya Mzee Mpilimi lililopo Kata ya Nala Halmashauri ya Dodoma Mjini, kwa ajili ya kusikiliza mgogoro huo ulioibuliwa na wanandugu wanaogombea mali za marehemu huku ikidaiwa Mtoto wake aitwaye Marco Mpilimi, amejilimbikizia mali za marehemu.
Aidha, Waziri Silaa, amewaagiza Makamishina Wasaidizi wa Ardhi wa Mikoa nchini kote kuacha mara moja kushughulikia mirathi na wasimamizi wasiokuwa na barua ya utambulisho wa mahakama.
Hata hivyo Waziri amekiri wazi baadhi ya migogoro ya ardhi imekuwa zigo kwa Serikali kwani familia zinayo nafasi ya kukaa pamoja na kutatua migogoro hiyo wao wenyewe.