Wadau wa maktaba kuu ya mkoa wa Tanga,wameiomba serikali kwa kushirikiana na wasamaria wema kuifanyia ukarabati miundo mbinu yake iliyojengwa enzi za wakoloni wa kiingereza 1956 kufuatia kuchakaa vibaya na kusababisha kipindi cha mvua baadhi ya maeneo kuvuja.
Mkutubi mkuu wa maktaba hiyo Martin Chambo amesema pamoja na mashirika wahisani kusaidia ukarabati katika baadhi ya maeneo,bado kuna changamoto kubwa kwa sababu maktaba hiyo imejumuishwa katika makumbusho ya kitaifa ili kuongeza idadi ya watalii kutoka uingereza kutembelea maktaba hiyo.
Katika zoezi hilo msaidizi wa maktaba ya mkoa Ester Lumambo amesema mbali na uchakavu wa miundo mbinu pia wanakabiliwa na changamoto ya machapisho mapya na kusababisha baadhi ya wanafunzi wa kuanzia elimu ya msingi hadi vyuo vikuu kushindwa kukidhi mahitaji.
Kufuatia hatua hiyo,wadau wa maktaba hiyo ,wasamaria wema kwa kushirikiana na serikali wameombwa kuikarabati maktaba hiyo kongwe nchini iliyopewa jina la kumbukumbu ya mfalme George wa Uingereza ambaye ni baba wa malkia Elizabert ili iweze kurejea katika uhalisia wake.