Mkazi wa Kamizilente Kagera atiwa Mbaroni kwa kukutwa na sare za JWTZ.
Jeshi la polisi katika mkoa wa Kagera linamshikilia Octovian Valentine Mengere mkazi wa mtaa wa Kamizilente katika halmashauri ya manispaa ya Bukoba ambaye ni mlinzi wa kituo cha afya cha Nshambya kilichoko katika manispaa akiwa amevaa sare za jeshi la wananchi wa tanzania (JWTZ) ambazo inadaiwa alikuwa akizitumia kuwatishia wananchi wanaoishi katika mtaa huo na maeneo mengine kwa kujifanya askari wa jeshi hilo.
kamanda wa jeshi la polisi mkoani kagera kamishina msaidizi mwandamizi revocatus malimi amesema mtu huyo amekamatwa kwenye eneo la machinjio yaliyoko kwenye mtaa wa Kamizilente na jeshi la polisi linaendelea kumhoji kujua hizo sare amezipata wapi pamoja na yeye kueleza kuwa amepewa na mmoja wa wauguzi wa kituo cha afya cha Nshambya.