Back to top

Mkoa wa Shinyanga wajiandaa kukabiliana na Corona.

01 July 2021
Share

Mkoa wa Shinyanga umejiandaa kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona kwa kutenga vituo maalum vya kutoa huduma kwa watu watakaohisiwa kuwa na maambukizi hayo.

Kauli hiyo imetolewa na mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt.Yudas Ndungile wakati Meneja wa Mradi wa Enrich unaotekelezwa na Shirika la World Vision akikabidhi msaada wa vifaa-kinga na tiba vyenye thamani ya Shilingi 126,260,000 kwa mkuu wa mkoa huo ,  lengo likiwa ni kusaidia kukinga na kutibu waginjwa watakaobainika.

Meneja wa mradi wa lishe wa Enrich, Bwana Frank Mtimbwa unaotekelezwa na World Vision katika mkoa wa Shinyanga na Singida amesema   malengo ya shirika hilo kutoa msaada huo ni kuiungs mkono serikali.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt.Philemoni Sengati ametoa hali halisi ya ugonjwa wa Covid-19 mkoani humo na kuitaka jamii kutofanya mzaha katika kutekeleza mikakati inayotolewa na serikali juu ya ugonjwa huo.