Back to top

Mkuchika asema Rushwa, ufisadi ni tatizo kwa viongozi Bara la Afrika.

15 August 2021
Share


Waziri asiye na Wizara maalum, Mhe.Kapteni Mstaafu George Mkuchika amesema rushwa, ulimbikizaji mali na ukandamizaji, bado ni tatizo kubwa kwa viongozi wa Bara la Afrika hali inayochangia kukwamisha maendeleo pamoja na ustawi wa nchi na watu wake.

Kapteni mstaafu Mkuchika ameyasema hayo wilayani Chato alipotembelea kaburi la aliyekuwa Rais wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli akiambatana na mkewe akimwelezea hayati Magufuli kuwa alipambana na rushwa waziwazi bila kumwogopa mtu.

Kapteni mstaafu Mkuchika amewataka viongozi waliopo madarakani kumuenzi hayati Magufuli kwa kuwatumikia wananchi na kutatua kero za wananchi ili kuondokana na utegemezi.

Kuhusu mradi wa umeme wa Julius Nyerere Waziri Kapteni mstaafu Mkuchika amesema kukamilika kwa mradi huo kutapunguza bei ya umeme pamoja na kufua umeme wa kutosha utakaofika kila kijiji.