Mkutano wa 1 wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umeanza leo mkoani Dodoma ambapo wabunge wamemchagua mbunge wa jimbo la Kongwa Job Ndugai kuwa Spika wa bunge hilo.
Uchaguzi huo umefanyika chini ya Uenyekiti wa mbunge wa jimbo la Isimani Willium Lukuvi ambaye aliteuliwa kusimamia kutokana na kuwa mmoja kati ya wabunge wenye uzoefu zaidi ndani ya bunge hilo.
Akitangaza matokeo hayo Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai amesema Mhe.Ndugai amepata kura 344 kati ya kura 345 zilizopigwa na wabunge hao na hivyo kuwa spika wa Bunge hilo.
Mhe.Ndugai alikuwa Spika katika Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.