Back to top

Mlima wa utalii wazinduliwa Mtwara.

09 June 2019
Share


Wakazi wa wilaya ya Masasi mkoani Mtwara wameingia katika historia baada ya kuzinduliwa rasmi kwa jabali kubwa la mlima Mkomaindo kuwa miongoni mwa vivutio vya utalii, ambapo katika jabali hilo kuna vivutio mbalimbali ikiwemo mapango,maeneo mazuri ya kustarehe pamoja na uwepo wa msalaba unaosadikika kujengwa na wamisionari mwaka1876.

Mlima Mkoamaindo una urefu wa zaidi ya mita 540 lakini pia kuna kumbukumbu ya msalama uliowekwa mwaka 1876 na wamisionari walioleta injili katika wilaya hiyo.

Baadhi ya wananchi na washiriki wa mbio za kupanda mlima huo  wanasema kuzinduliwa kwa jabali hili ndio mwanzo wa kutambua vivutio mbalimbali katika wilaya hiyo.

Katika uzinduzi huo kumeshuhudiwa michezo mbalimbali mvuto ukibaki kwa washindani wa kupanda mlima pamoja na vikwazo mbalimbali mchezo ulioandaliwa na vikosi vya ulinzi na usalama.