Back to top

MOI yafanya upasuaji katika ubongo wa binadamu kutibu kifafa.

14 November 2019
Share

Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) kwa mara ya kwanza imefanya upasuaji mkubwa katika ubongo wa binadamu kwa ajili ya kutibu ugonjwa wa Kifafa.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, katika chumba cha upasuaji, Dkt.Japhet Ngerageza amesema, huo ni upasuaji wa kwanza na umemuhusisha mtoto ambaye alisumbuliwa na Kifafa kwa miaka minne.

Naye Dakitari Bingwa wa upasuaji kutoka Canada, Dkt.Evan Lewis amesema upasuaji huo katika hali ya kawaida ungechukua saa mbili,  lakini kwa saabua ni mara ya kwanza kufanyki hapa nchini, umechukua saa tatu ili kutoa fursa kwa wataalam wa hapa nchini kufuatilia  kwa kina.

Daktar bingwa wa Dawa za Usingizi, Dkt.Karima Khaleed amesema imekuwa ni jambo jema kushiriki katika upasuaji huo na cha msingi walichokuwa wanakizingatia zaidi ni kuangalia umri wa mtoto na kiasi halisi cha dawa ambacho anapswa kupewa.