Wasomi wote nchini wametakiwa kubadili fikra zao kwa kutumia akili vumbuzi na sio akili kibarua ili kulisaidia Taifa kusonga mbele kwa maendeleo.
.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, Bungeni Jijini Dodoma, wakati akijibu swali la Mbunge kutoka Baraza la Wawakilishi, Mhe. Ameir Abdallah Ameir, aliyeuliza Je, ni tafiti zipi ambazo Taasisi za Tiba Asili zimekamilisha na kuweza kuwa suluhisho la maradhi mbalimbali kama tiba mbadala.
.
Dkt. Mollel amesema, katika kipindi cha kuanzia mwaka 2021 hadi 2024, zaidi ya tafiti 50 zimefanyika ndani ya nchi, juu ya ubora na usalama wa dawa zinazotumika kwa tiba asilia kwa kupitia Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR).
.
Ameongeza kuwa baadhi ya tafiti hizo ni pamoja na utafiti wa dawa ya Saratani ya NIMREGENIN, Dawa ya TANGHESHA inayotibu Selimundu, Dawa ya PERVIVIN inayotibu tezi dume, Dawa ya WARBUGISTAT inayotibu magonjwa nyemelezi na Dawa ya NIMRICAF inayotibu Mfumo wa upumuaji.