Back to top

Moto waua watu watano wa familia moja Pugu.

14 October 2020
Share

Watu watano wa familia moja akiwemo mama, watoto wake watatu pamoja na fiwi yake wamepoteza maisha baada ya nyumba yao kuwaka moto majira ya saa nne usiku wa kuamkia leo katika eneo la Pugu CCM Kirumba jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika mahojiano maalum na ITV Online baba wa familia hiyo Edward katemi amesema moto huo ulianza majira ya Saa nne usiku na waliofariki katika familia hiyo ni Mke wake Jackline Frank, mdogo wake Ester Katemi na watoto wake Edwin Katemi, Edson katemi pamoja na Evon Katemi.

Bw.Edward amesema kwa kushirikiana na majirani zake walipambana kuiokoa familia yake bila mafanikiko kutokana na ukosefu wa vifaa vya kuwezesha uokoaji katika tukio hilo na waliwasiliana na watu wa kikosi cha uokoaji lakini walichelewa kufika kutokana na changamoto ya usafiri iliyokuwepo.

Kamanda wa polisi Ilala amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema watu hao walifanikiwa kuokolewa na kukimbizwa hospitali lakini kwa bahati mbaya walipoteza maisha na chanzo cha moto bado hakijafahamika japo moto huo ulianzia sebuleni.