Back to top

Msijenge chuki na Askari wa usalama barabarani

28 August 2022
Share

Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani Mkoa wa Mtwara limesema hakuna haja ya kujenga chuki na Askari wa usalama barabarani na badala yake jamii iwe tayari kutoa taarifa pale inapoona haitendewi haki na baadhi ya askari wa usalama barabarani.
.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Mtwara ACP George Shimba wakati akitoa elimu ya usalama barabarani kwa watumishi wa kituo cha utafiti wa kilimo TARI Naliendele.
.
Amesema  jeshi la polisi linafanya kazi kwa ukaribu na wananchi hivyo ni vema  kuendelea  kuheshimu ushikiriano huo na kuwa tayari kutoa taarifa iwapo kuna baadhi ya askari wa usalama barabarani hawatendi haki kwa madereva wawapo barabarani.
.
Hata hivyo amewasihi madereva kuheshimu sheria za usalama barabarani  ili kupunguza ajali za zinazotokea ambapo takwimu zinaonyesha kuwa asilimia sabini na sita ya ajali hizo zinatokana na uzembe wa madereva.