Mwili wa aliyekuwa mtangazaji wa Clouds Media Group Bwana Ephraim Kibonde aliyefariki Machi 7, 2019 jijini Mwanza utaagwa kesho saa 4 asubuhi nyumbani kwa wazazi wake Mbezi na kisha kwenda kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Msemaji wa familia Bw.Boniface Mwakijolo amesema mwili wa marehemu Ephraim utawasili kesho kutokea hospitali ya Lugalo na kisha ibada ya kumuaga ndugu yao itafanyika
Naye Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kifo cha Ephraim Kibonde ni pigo kubwa kwa taifa, Clouds Media Group na tasnia ya habari kwa ujumla, Amesema hayo alipokwenda kuhani msiba huo kwa niaba ya Rais Dkt.John Magufuli.