Mwenyekiti wa Chama Cha NCCR Mageuzi Taifa Mhe. James Mbatia amesema chama chake kitaendelea kusimamia siasa za maridhiano katika kuhakikisha kuwa Tanzania inafikia Lengo la kufikia maendeleo yanayoigusa jamii yote kuanzia ngazi ya chini.
Mhe. Mbatia ameyasema hayo jijini Arusha akizumgumza na Wanachama wa NCCR Mageuzi kutoka wilaya mbalimbali za Mkoa wa Arusha akisisitiza Watanzania kuishi kwa maneno ya Hayati Dakta Reginald Mengi aliyosisitiza Amani kwa kuepuka maneno yanayoweza kuvunja Amani.