Back to top

Ndalichako ataka uchunguzi ujenzi wa chuo cha VETA Kagera.

10 January 2021
Share

Waziri wa Elimu, Prof.Joyce Ndalichako amemuagiza Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu ya Ufundi na Stadi (VETA) Dkt.Peter Maduki kuunda kamati ya wataalam itakayochunguza thamani halisi ya fedha ambayo imetumika kwenye mradi wa ujenzi wa chuo cha VETA unaofanywa  mkoani Kagera wilayani Karagwe na wakala wa majengo nchini (TBA) kama inalingana na hatua ya mradi ambayo imeshafikiwa na kiwango cha mradi huo.

Profesa ndalichako ambaye pia ameshuhudia zoezi la kutia saini mkataba wa halmashauri ya wilaya ya Karagwe kukabidhi chuo cha ufundi cha halmashauri hiyo kwa VETA, ametoa agizo hiyo baada ya kukagua mradi huo na kuonyesha kutoridhishwa na uwiano wa fedha ambayo imeishatolewa na hali halisi ya mradi. 

Kwa upande wake, mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti ameomba mamlaka hiyo ianze kuandaa mafunzo maalumu kwa vijana ili waweze kunufaika na mradi wa ujenzi la mafuta. 

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa VETA, Dkt.Pancras Bujulu amesema mradi huo utagharimu zaidi ya shilingi bilioni 4.6, huku mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Karagwe Godwin Kitonka akisema chuo hicho kwa kumilikiwa na VETA kitawanufaisha zaidi wananchi.