Back to top

NDENJEMBI KUMUWAJIBISHA AFISA ARDHI KWA KUKOSA UADILIFU

31 August 2024
Share

 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe Deogratius Ndejembi, amemuelekeza Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi,  kumchukulia hatua za kinidhamu Afisa Ardhi Msaidizi Mwandamizi, Bw. Emmanuel Segeja kwa kukosa uadilifu na kuleta taharuki iliyosababisha mgogoro wa ardhi wa viwanja viwili vilivyopo Bahari Beach, Dar es Salaam.

Mhe. Ndejembi amechukua hatua hiyo baada ya kupokea malalamiko ya wananchi hao wenye mgogoro na kufika kusikiliza pande zote mbili na kugundua kuwa Afisa huyo aliruhusu upimaji wa ardhi hizo juu ya upimaji mwingine bila kufuata utaratibu na kupelekea watu kupewa hati miliki nyingine juu ya viwanja hivyo.

Aidha Mhe. Ndejembi ameelekeza shughuli za ujenzi katika eneo hilo zisimame hadi hapo suluhu ya mgogoro huo itakapopatikana. Katika ziara hiyo Mhe Ndejembi ameambatana na Naibu Katibu Mkuu, Bi. Lucy Kabyemera pamoja Kamishna wa Ardhi, Mathew Nonge.