Baraza la taifa la uhifadhi na usimamizi wa mazingira nchini Tanzania (NEMC) imefunga machinjio ya nyama ya msalato na kuitoza halmashauri ya jiji la Dodoma faini ya sh 5 milioni.
Hatua ya kufungwa kwa mnada huo imekuja baada ya kamati ya bunge ya viwanda, biashara na mazingira kufanya ziara katika machinjio hayo ambayo huhudumia mnada maarufu wa Msalato ambao hufanyika kila Jumamosi ambapo Mkurugenzi mkuu wa NEMC Dk Samwel Gwamaka amesema hawataifungua machinjio hiyo hadi pale watakapojiridhisha kuwa imekamilisha vigezo.
Baadhi ya wananchi wamesema wamekuwa wakitegemea machinjio hayo kwa ajili ya kuwaingizia kipato ambapo wameiomba halmashauri ya jiji la Dodoma kuboresha hali ya mazingira katika eneo hilo.