![](https://www.itv.co.tz/sites/default/files/styles/large/public/field/image/231024141530-cat-china-file-restricted.jpg?itok=LLiRkACn)
Polisi nchini China wamewaokoa paka 1,000 kutoka kwenye lori lililokuwa likielekea kwenye machinjio, na pia kuharibu sehemu ya biashara haramu, inayouza kwa njia ya udanganyifu nyama ya paka kama nguruwe au kondoo na kuzua wasiwasi wa usalama wa chakula.
Wanaharakati wa wanyama mapema mwezi huu, maafisa kutoka Zhangjiagang, katika jimbo la Mashariki la China la Jiangsu, walinasa gari lililokuwa likitumika kukusanya na kusafirisha paka waliokamatwa.
Ripoti inasema gari hilo lilikuwa linaelekea katika machinjio hivyo kuna uwezekano mkubwa wa paka hao walikuwa wanapelekwa kuchinjwa na kusafirishwa Kusini ili kutumiwa kama mishikaki ya nguruwe na kondoo pamoja na soseji.