Back to top

Raia 11 wa nchi ya Burundi wakamatwa na polisi kwa kulima bangi.

21 April 2019
Share

Raia 11 wa nchi ya Burundi wanashikiliwawa na jeshi la polisi wilayani Kasulu Mkoani Kigoma Baada ya kukutwa katika hifadhi ya Msitu wa Makere Kaskazini wilayani humo wakilima zao haramu la Bangi.

Watuhumiwa hao wamekamatwa na vikosi vya ulinzi vya wakala wa huduma za Misitu Tanzania (TFS) wilayani Kasulu, wakati wa operesheni inayoendelea ya kufyeka na kuteketeza Bangi ndani ya hifadhi hiyo.

Mkuu wa wilaya ya Kasulu  Kanal Simon Anange amesema mpaka sasa wana zaidi ya ekari 30 za bangi zilizo gunduliwa na kuharibiwa katika hifadhi ya Msitu wa Makere Kasikazini huku mashamba hayo yakidaiwa kulimwa na watanzania na Warundi na watuhumiwa watafikishwa mahakamani.

Kufuatia hali hiyo, Kanal Simon Anange ametoa onyo Kwa raia wa nchi Jirani na wakimbizi waliopo wilayani hutojihudisha na uhalifu.