Back to top

Rais Kenyatta wa Kenya athibitisha watu wawili kuwa na Corona.

15 March 2020
Share

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amefunga shule zote nchini humo kutokana na kuongezeka kwa watu wawili ambao wamepatikana na virusi vya Corona nchini humo.

Watu hao wawili walikuwa wametangamana na mgonjwa wa kwanza aliyepatikana na virusi hivyo.

Idadi hii inafanya idadi ya visa vya coronavirus nchini Kenya kufikia watu watatu. Hata hivyo amesema wagonjwa wako katika hali nzuri na hilo linatupa matumaini.

Akizungumza Wakenya kupitia televisheni Rais Kenyatta amesema masomo katika shule taasisi zote yamesimamishwa mara moja, huku shule za msingi na sekondari zitafungwa kuanzia Jumatatu huku za bweni zitafungwa ifikapo Jumatano.

Vyuo vikuu na vyuo pamoja na taasisi nyingine za elimu zitafungwa ifikapo Ijumaa na pale inapowezekana waajiriwa wanapaswa kuruhusiwa kuhfanya kazi nyumani kwao ili kuepukana na maambukizi ya coronavirus.

Amesema watu wote walioingia Kenya raia au wageni watatakiwa kujitenga kwa muda wa siku 14 na yeyote atayekuwa na joto la juu la mwili ajipeleke kwenye kituo cha afya.

Kulingana na tamko la rais huyo ni raia wa Kenya tu na wakazi wa kigeni wenye visa halali watakaokubaliwa kuingia nchini Kenya kwa muda wa siku 30 zijazo ili kuepuka maambukizi ya virusi vya corona.

''Ili kuepuka maambukizi kwa njia ya pesa tunashauri watu watumie njia ya matumizi ya pesa ya mobile, credit bank, na tunazitaka benki ziangalie jinsi ya kupunguza viwango tozo za matumizi ya simu za mkononi ya pesa'', amesema Bwana Kenyatta ambaye amewataka Wakenya kuwa watulivu.

Huku akiainisha agizo lake hilo kwa vipengele Bwana Kenyatta amesema kwa mujibu wa agizo la kuepuka maeneo yenye mikusanyiko mikubwa, watu waepuke maeneo yenye umati wa watu, agizo lake likisema watu :