
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan kesho tarehe 28 Machi, 2021 atapokea taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) za mwaka wa fedha 2019/20 na taarifa ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ya mwaka 2019/20.
Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu kwa vyombo vya habari imeeleza kuwa hafla ya kupokea taarifa hizo itafanyika Ikulu, Chamwino Mkoani Dodoma kuanzia saa 4:00 Asubuhi.