Back to top

RAIS MWINYI NA PRINCESS SOPHIE WATETA IKULU

19 September 2024
Share

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, amekutana Princess Sophie (Duchess of Edinburgh)Ikulu Zanzibar, ambapo  ameihakikishia Uingereza kwamba Zanzibar inaendelea na mikakati na juhudi kubwa ya kuhakikisha inadhibiti na kuumaliza ugonjwa wa Trakoma (Trachoma) nchini.


Aidha, Dk. Mwinyi amesema hatua iliyofikiwa na Zanzibar ya kukabiliana na magonjwa mbalimbali inatokana na juhudi kubwa na misaada ya afya inayotolewa na Uingereza, na kumuahidi kuwa Zanzibar itaendelea kufanya kazi kwa bidii ili kupambana na magonjwa, hasa yasiyoambukiza (NCDs), yanayoathiri ustawi wa jamii.

Kwa upande wake Princess Sophie, ameipongeza Zanzibar kwa hatua iliyofikia ya kudhibiti ugonjwa wa Trakoma kwa kiasi kikubwa na kufikia mapema malengo yaliyowekwa na Jumuiya ya Madola, ya kumaliza ugonjwa huo ifikapo mwaka 2030.


Princess Sophie ni Mke wa Prince Edward, mtoto wa mwisho wa Malkia Elizabeth II,na mdogo wa Mfalme wa Uingereza wa sasa  Charles III, kwa sasa yupo Zanzibar kwa ziara ya siku sita, kutembelea miradi mbalimbali ya Afya inayotekelezwa na Taasisi tofauti ambazo yeye ni mlezi wake.