Back to top

RAIS SAMIA AONGEZA DAU, SASA GOLI NI MIL.10

28 April 2023
Share

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ametangaza kuongeza fedha za motisha kwa timu za Simba na Yanga kutoka shilingi milioni 5 hadi milioni 10 kwa kila goli , endapo timu hizo zitafuzu kucheza nusu fainali za mashindano ya CAF.
.
Hayo yamesemwa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, ambapo amebainisha kuwa motisha hiyo itatolewa kwa magoli yatakayofungwa katika dakika 90 za mchezo au dakika 120 na sio magoli ya penati.