Rais wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan, amewatakia kila la kheri wanafunzi wote wa darasa la saba wanaoanza mitihani yao ya kuhitimu elimu ya msingi leo Septemba 13, 2023 na kuwahakikishia kuwa serikali imekamilisha maandalizi ya miundombinu ya kuwapokea wote watakaoendelea na kidato cha kwanza mwaka 2024.
Rais Samia amesema 'Nawatakia kila la kheri wanafunzi wote wa Darasa la Saba wanaoanza mitihani yao ya kuhitimu leo. Mmefikia hatua muhimu ya safari yenu ya awali, kuelekea njia mtakazochagua siku za usoni katika kutoa mchango wenu kusukumu mbele gurudumu la maendeleo ya Taifa letu'
Nawaombea kwa Mwenyezi Mungu aliyewasimamia toka mwanzo wa safari hii ya elimu hadi sasa, akawape utulivu na afya njema, ili mfanye vizuri mitihani yenu.
Serikali tayari imekamilisha maandalizi ya miundombinu ya kuwapokea wote mtakaoendelea na kidato cha kwanza mwaka 2024.