Back to top

Rais Samia kuhutubia bunge Aprili 22.

19 April 2021
Share

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan anatarajia kulihutubia bunge Aprili 22 mwaka huu na kuelezea malengo na mwenendo mzima wa serikali yake ya awamu ya sita hotuba ambayo ataitoa majira ya saa kumi Alasiri.

Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai ametoa taarifa hiyo kwa wabunge bungeni jijini Dodoma na kuwataka wabunge wotekufika bungeni siku hiyo ya Alhamisi ili kumsiliza rais ambapo marais wote wastaafu ni miongoni mwa viongozi walioalikwa kudhuria hotuba hiyo.