Back to top

Rais wa Kenya aidhinisha sheria mpya ya mitandaoni.

16 May 2018
Share

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameidhinisha Mswada wa Sheria za Uhalifu Mtandaoni wa 2018 kuwa Sheria,hatua itakayotoa adhabu kali kwa watakaopatikana na makosa ya mtandaoni.

Sheria hiyo inatoa adhabu ya faini ya Sh5 milioni (dola 50,000 za Marekani) au kifungo cha miaka miwili jela,au adhabu zote mbili,kwa atakayepatikana na kosa la uenezaji wa habari za uzushi.

Mtu atakayepatikana na kosa la kueneza taarifa ambazo zinaweza kuzua taharuki au kuzua vurugu atafungwa jela zaidi ya miaka kumi.

Sheria hiyo inatarajiwa kuathiri utendakazi wa wanahabari,vyombo vya habari, watumiaji wa mitandao ya kijamii,wanablogu na watu wengine wanaotumia kompyuta na mitandao.