Back to top

Rais Zambia aongoza maombolezo ya samaki maarufu kama 'Mafishi'.

08 September 2020
Share

Rais Edgar Lungu ameungana na Chuo Kikuu Cha Umma cha Copperbelt (CBU) kuomboleza kifo cha samaki mkubwa aliyekuwa akiishi katika bwawa la chuo hicho aliyejulikana kwa jina la mafishi aliyefariki usiku wa kuamkia Septemba 08.

Baadhi ya wanafunzi walikuwa wakimtembelea samaki huyo kabla ya kufanya mtihani wakiamini kuwa kufanya hivyo kunawasaidia kufanya vizuri katika mitihani huku Wanafunzi wengine wakisema samaki huyo aliwasaidia kujiondolea msongo wa mawazo.

Wanafunzi waliomboleza kifo cha samaki huyo kwa kuwasha mishumaa huku vilio vikitawala.