Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya jamii TASAF,Bw. Ladislaus Mwamanga,amesema serikali ilianzisha TASAF mwaka 2000 kama moja ya jitihada za kupunguza umaskini kwa wananchi wake wanaoishi kwenye hali duni.
Akizungumza na ITV Mwakilishi wa Mkurugenzi huyo, Hamisi Kikwape,amesema muda wa utekelezaji mpango ni kipindi cha miaka kumi ambapo umegawanywa katika awamu mbili za miaka mitano na umeshaandikisha kaya maskini zaidi ya Milioni moja zinazoishi katika hali duni kwenye vijiji na mitaa yetu.