Serikali imesema ipo katika mchakato wa kurekebisha sheria inayohusiana na likizo ya uzazi iendane sambamba na hali halisi ya mzazi husika na mtoto aliyezaliwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama ameliambia bunge kuwa hilo linatokana na baadhi ya wazazi kujifungua watoto kabla ya wakati hivyo huitaji matunzo ya kipekee.
Amesema mzazi wa namna hiyo hutakiwa kupumzika zaidi kuliko yule anayejifungua kwa wakati ili kumfanya aweze kumlea vyema mwanae.
Waziri Mhagama alikuwa akijibu swali bungeni kuhusiana na likizo ya uzazi kutokutenda haki kulingana na namna ambavyo mzazi husika amejifungua.