Back to top

Serikali yaombwa kujenga kivuko kuwanusuru wananchi kuliwa na Mamba.

16 January 2021
Share

Wananchi wa vijiji vya Mngeta na Isango katika halmashauri ya wilaya ya Mlimba wilayani Kilombero wameiomba serikali kuwajengea kivuko salama kwenye mto Mngeta kwa ajili ya kuunganisha vijiji hivyo na kuwarahisishia kufuata huduma za Afya na Elimu kutokana na muda mrefu kutumia mtumbwi mmoja uliopo kuvuka mto huo.

Hatua hiyo inatokana na eneo hilo kutokuwa salama kutokana na wingi wa mamba wanaojeruhi na hata kusababisha vifo kwa baadhi ya wakazi.