Baada ya ITV/Radio One kuibua changamoto ya ufinyu wa bajeti ya ukarabati wa barabara ya Mbalizi - Mkwajuni iliyoathiriwa na mafuriko katika eneo la kanga wilayani Songwe, serikali imeongeza fedha za kujenga madaraja mengine 3 na kufanya jumla yake kuwa 7 ikiwa ni pendekezo la wahandisi wa TANROADS na mkandarasi waliodai madaraja 4 yanayojengwa hayatatosha kuikabili nguvu ya Mafuriko yanayotokea.
Naibu Waziri wa Ujenzi Eng.Godfrey Kasekenya ametembelea eneo la mradi na kuwahakikishia wananchi kuwa barabara hiyo itaimarika kwa wakati mwafaka na kutumika kabla mvua hazijaanza kunyesha.
Aidha, Mkuu wa Wilaya Songwe, Simon Simalenga amesema chanzo cha kutokea kwa mafuriko hayo ambacho ni ukuta wa mto zila kubomoka na kuchepusha njia ya maji kitadhibitiwa ili maji yafuate mkondo wake wa asili, Mto Zilla.