Tume ya uchaguzi ya Zanzibar imepitisha sheria mpya ambapo kwa mara ya kwanza uchaguzi mkuu kwa upande wa Zanzibar baadhi ya wadau wataruhusiwa kupiga kura siku moja kabla ya siku yenyewe.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ya Zanzibar Jaji mkuu Mstaafu Hamid Mahmud wakati akizindua sheria hiyo kwa viongozi wa vyama vya siasa 19 na wadau wa sekta za jamii katika mkutano wa pamoja ambapo amesema kwa kuanzia utaratibu huo ni watendaji wa tume na askari watakaohusika na ulinzi na usalama wa siku ya upigaji kura.