Shirika la Masoko ya Kariakoo limesema kuwa mradi wa ujenzi na ukarabati wa Soko la Kariakoo, bado unaendelea na hakuna eneo la biashara lililopangishwa kwa mfanyabiashara yeyote hadi sasa.
Shirika hilo limekanusha taarifa zisizo rasmi, zinazosambaa kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, kuwa tayari Soko la Kariakoo limeanza kupangisha maeneo ya biashara.
Shirika hilo pia limesema, taarifa rasmi kuhusu upangishaji wa maeneo yote ya biashara katika Soko la Kariakoo, zitatolewa na Uongozi wa Shirika baada ya mradi kukamilika