Back to top

Sokwe mtu wako hatari ni kutoweka Kigoma.

15 July 2018
Share

Wanyama adhimu duniani sokwe mtu wako hatarini kutokweka kutokana na shughuli za kibinadamu zinazoendelea kandokando ya Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale mkoani Kigoma inayohifadhi wanyama hao ambazo ni pamoja na uchomaji moto misitu, kilimo holela na uwindaji.

Mhifadhi Mwandamizi katika Hifadhi ya Sokwe  ya Milima ya Mahale Peter Maziku  amesema vitendo vya uchomaji wa misiti vimekuwa vikisababisha maisha ya sokwe mtu kuwa magumu .

Mkuu wa wilaya ya Uvinza Mwanamvua Mrindoko ameagiza wakati wa Maadhimisho ya siku ya Sokwe duniani katika kijiji cha Mgambo kata ya Buhingu inayopakana na hifadhi hiyo, viongozi wa vijiji na kuhakikisha wanasimamia kikamilifu sheria ndogo za utunzaji wa mazingira sambamba na kuwachukulia hatua wanaobainika kuchoma moto mapori na kusababisha uharibifu wa mazingira.