Back to top

TAMISEMI YATANGAZA AJIRA 21,200, UALIMU NA AFYA

12 April 2023
Share

Wizara ya TAMISEMI imetangaza kuajiri watumishi 21,200 wa Kada za Ualimu na Afya, ambapo Wizara hiyo imesema watakaoajiriwa katika kada ya Ualimu ni 13,130 ambao watafundisha katika shule za Msingi na Sekondari, huku 8,070 wakiwa ni kada ya Afya, ambao watafanya kazi katika Hospitali za Halmashauri, Vituo vya Afya na Zahanati.
.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Angellah Kairuki, ambapo amesema hatua hiyo imefuata baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuridhia kutoa kibali cha ajira hizo. 
.
Waombajiwa ajira hizo wanatakiwa kuwa wale waliohitimu kuanzia mwaka 2015 hadi 2022 ambapo wanatakiwa kutuma maombi yao kwa njia ya mtandao kupitia kiunganishi cha ajira.tamisemi.go.tz, kuanzia leo Aprili 12, 2023 hadi Aprili 25, 2023, saa 05:59 usiku.