Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetangaza kutoa zawadi kwa watakaofanikisha kupatikana kwa vyuma vilivyoibiwa kwenye nguzo kubwa za umeme(Towers) zilizopo Kata ya Busale wilayani Kyela mkoani Mbeya na kusababisha nguzo nne kuanguka na hasara ya Shilingi milioni 900 huku baadhi ya maeneo ya Mji wa Kyela yakikosa umeme kutokana na wizi huo.