Back to top

TANZANIA NI SEHEMU SALAMA KWA BIASHARA NA UWEKJEZAJI

02 July 2024
Share

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Abdul-Razaq Badru, amesema mfuko huo unashiriki katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam ili kutoa huduma kwa wananchama wake lakini pia kuunga mkono jitihada za serikali katika eneo la biashara na uwekezaji.

Bw. Badru ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la Mfuko huo kuhusu ushiriki wa PSSSF kwenye Maonesho hayo.

“Pamoja na kutoa huduma za wanachama pia tunawekeza katika maeneo mbalimbali, na kama kaulimbiu inavyosema, Tanzania ni sehemu salama kwa biashara na uwekjezaji, na sisi PSSSF tuko hapa kwenye Maonesho haya ili kuwaeleza wanachama na wananchi kwa ujumla fursa zilizopo katika uwekezaji uliofanywa na Mfuko, tumewekeza kwenye majengo ya kupangisha ofisi,maduka, migahawa, nyumba za bei nafuu lakini pia viwanja kwa wale wenye uhitaji.” Mkurugenzi Mkuu PSSSF Bw. Abdul-Razaq Badru.