Back to top

BITEKO: VYAMA VYA USHIRIKA ONGEZENI UBUNIFU.

06 July 2024
Share

Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko amevitaka vyama vya ushirika kubuni mbinu mpya, zitakazowezesha wakulima kupata huduma, pembejeo na bei bora za mazao yao ili kuchochea maendeleo.

Dkt. Biteko amesema hayo wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani  (SUD),  yaliyofanyika katika Viwanja vya Ipuli mkoani Tabora ambapo amesema umefika wakati wa kufanya mabadiliko ya dhati, katika sekta ya Kilimo na kuondokana na michakato na maoni yasiyo na tija ambayo huchelewesha maendeleo.

Amevitaka vyama vya ushirika na wanunuzi wa mazao kuhakikisha wanarejesha rasirimali kwa wananchi kupitia CSR ili maendeleo katika maeneo husika yaendane na rasiriamali zinazopatikana katika maeneo hayo.